Events

Chalamila: TRA toeni elimu kwa mlipa kodi

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya oparesheni maalum ya elimu kwa mlipa kodi nchini ili kusaidia kukusanya mapato kwa kiwango kikubwa.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha kuhamasisha ulipaji kodi awamu ya nne na kubainisha kuwa miongoni mwa vitu vinavyoiongoza nchi ni ukusanyaji kodi kwa kufuata sheria na utaratibu uliowekwa.

Awali akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TRA Edmund Kawamala Naibu kamishna kodi za ndani divisheni ya walipa kodi wadogo amesema makusanyo ya kodi nchini yanategemea Mkoa wa Dar es salaam maana ndio mkoa wa kitivo cha biashara na walipa kodi wengi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya kinondoni, Saad Mtambule amesema wataendelea kushirikiana na TRA kwa karibu katika Wilaya hiyo ili waweze kuwafikia walipa kodi na kukusanya mapato ya Serikali kikamilifu.