Join us

FOMU YA MAOMBI YA UANACHAMA

Kumbuka:(Fomu hii ijazwe kwa herufi kubwa)

1. SIFA ZA KUJIUNGA NA CHAMA

i. Awe mlipakodi anayetambulika na mamlaka ya mapato Tanzania.
ii. Mwanachama anaweza kuwa Taasisi, Kampuni, Kikundi au Mtu binafsi.

2. WAJIBU WA MWANACHAMA

i. Wajibu wa kulipa kodi stahiki.
ii. Wajibu wa Kuhudhuria vikao vyote vya Chama.
iii. Wajibu wa Kuchangia michango yote ya chama kama itakavyothibitishwa na
Mkutano Mkuu.
iv. Wajibu wa kuheshimu katiba na kanuni zote za chama kama ilivyoainishwa kwenye
katiba ya Chama cha Walipakodi Tanzania.
v. Wajibu wa kufichua wahujumu wa mapato ya Kodi.

3. HAKI ZA MWANACHAMA

i. Haki ya kutoa maoni.
ii. Haki ya kuhoji mapato na matumizi ya chama.
iii. Haki ya kupiga kura na kupigiwa kura.
iv. Haki ya kuishauri Serikali kuhusiana na masuala ya Kodi.
v. Haki ya kuhoji viwango vya kodi zinazowekwa na Serikali kwa kupitia vikao vya
chama.

4. MANUFAA YA KUJIUNGA NA CHAMA CHA WALIPA KODI TANZANIA

i. Chama kitakuwa rafiki wa karibu katika kutoa Elimu ya kodi, kufundisha sheria za
kodi,aina za kodi na jinsi kodi zinavyokadiriwa na namna ya kutatua changamoto za
kikodi.
ii. Chama kitasimama bega kwa bega na Mwanachama atakapokuwa na changamoto
za Kikodi.
iii. Chama kitatoa wataalamu wa mahesabu watakaokusaidia kuandaa mahesabu
yanayotakiwa kuwasilishwa TRA.
iv. Chama kitatoa jopo la wanasheria wa kodi watakao toa utetezi wa maswala ya Kodi
Mahakamani.
v. Chama kitasimama na Mwanachama wa hali zote ,bila kujali daraja lako la kiuchumi
ili kulinda haki na kutetea maslahi ya mwanachama.
vi. Chama kitapigania unafuu wa kodi ikiwemo kupunguza utitiri na viwango vya Kodi.
vii. Chama kitapaza sauti kwa niaba ya Mwanachama pale usiposikika kwa kupinga
uonevu na kudhibiti mfumo kandamizi katika ukusanyaji wa Kodi.

FOMU YA MAOMBI YA MWANACHAMA

A. MAELEZO BINAFSI YA MWOMBAJI

1.  (a) Jina Kamili la Mwombaji


Majina kamili ya mwakilishi wa Taasisi


Majina kamili  ya Kampuni


(b) Daraja la Mlipakodi


NOTE:

Viambatanisho:-
i. Cheti cha Usajili.
ii. Cheti cha Mlipakodi


2. TAARIFA YA KAZI/BIASHARA


3. TAARIFA ZA MAWASILIANO


B. UTHIBITISHO WA MWOMBAJI

 

Nathibitisha kwamba taarifa nilizotoa hapo juu ni kamili na sahihi kwa kadri ya ufahamu
wangu.


C: KWA MATUMIZI YA OFISI TU

 

KUPOKELEWA UANACHAMA:


 

Uthibitisho wa Mwanachama wa TATA


 

B. Malipo ya ada ya uanachama


C. Jina na Saini ya Viongozi wa Chama