EventsLatest News

Mamlaka ya Mapato Tanzania imekusanya kiasi shilingi za Kitanzania Trlioni 27.64/- kwa mwaka wa fedha 2023/2024

Mamlaka ya Mapato Tanzania  imekusanya cha shilingi za kitanzania Trilioni 27.64/- katoka mapato ya kodi kwa mwaka wa fedha wa 2023-2024 sawa na asilimia 97.67 ya lengo la kukusanya shilingi za kitanzania Trilioni 28.30.Makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 14.50 ikilinganishwa na trilioni 24.14/- zilizokusanywa mwaka wa fedha fedha uliopita, 2022-2023.

Hii ni baada kukusanya kukusanya kiasi cha shilingi shilingi za kitanzania Trilioni 7.09/- kwa robo ya nne, kuanzia Aprili hadi Juni 2024, na kufikia asilimia 99.46 ya malengo ta kukusanya kiasi cha  shilingi za kitanzania Trilioni 7.13 katika robo ya nne.

Akizungumzia hilo, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania  Alphayo Kidata, amesema miongoni mwa mambo yalichangia ongezeko hilo ni pamoja na kuongezeka kwa watalii na kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji katika biashara kuliko chagiza uagizaji wa  bidhaa kutoka nje ya nchi. Pia alibainisha kuwa mwitikio chanya kutoka kwa walipakodi wengi katika kuwasilisha marejesho na kulipa kodi kwa wakati umechangia ongezeko hilo.

Aidha, alitoa wito kwa walipakodi na wananchi kwa ujumla kutoa au kudai risiti za kielektroniki (EFD) pale wanaponunua bidhaa na huduma. Pia, aliwakumbusha  kuthibitisha uhalali wa Stamps za Kodi za Kielektroniki (ETS) kwenye bidhaa husika.

Swali kubwa, je kwa kiwango gani ongezeko hilo limeathiri uchumi wa kila mwananchi na Taifa kwwa ujumla? Toa maoni yako kupitia mitandao yetu ya kijamii au kupitia kiunganishi hiki https://tata.or.tz/submit-an-issue-form/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *