Majukumu ya Chama

a. Kuweka utamaduni endelevu kati ya walipakodi na mamlaka za kodi ambao utaimarisha ulipaji kodi wa hiari.
b. Kuratibu mikutano ya usuluhisho kati ya walipakodi na mamlaka ya Mapato kuhusu masuala ya Usimamizi wa kodi
c. Kuendesha semina, warsha na mafunzo mbalimbali yanayohusiana na masuala ya usimamizi wa kodi nchini.
d. Kuandaa na kuratibu mikutano/majukwaa ya wadau kuhusu haki za walipakodi;
e. Kushirikisha watumishi wa TATA,wanachama na wadau wengine katika kusaidia kutatua migogoro na changamoto zinazohusiana na uhiari wa ulipaji kodi, pamoja na kuwakilisha wanachama mbele ya mamlaka za mapato au jukwaa lolote ambapo uwakilishi huo unaruhusiwa kisheria;
f. Kuchukua hatua zote muhimu ili kuunda uhusiano mzuri kati ya walipakodi na mamlaka za Mapato.
g. Kushikilia, kupitia wadhamini wake, mali zinazohamishika na zisizohamishika, ambapo milki hiyo itaendeleza kazi za chama pamoja na ukuaji wa kijamii, kiuchumi na kiutamaduni wa Tanzania.
h. Kukuza uelewa na ufahamu wa umma juu ya haki na wajibu wa walipakodi ambao wanaweza kuhusika kufanya maamuzi sahihi pamoja na kushiriki katika uundaji na uboreshaji wa sera mbalimbali hususan za kodi na za ustawi wa walipakodi na kulinda haki zao;
i. Kuunda kwa mujibu wa Katiba chombo na vyama vinavyofanana nacho kama itakavyoona inafaa kwa ajili ya kutekeleza majukumu na kuendeleza malengo yake.
j. Kupokea michango toka kwa wanachama, msaada wa kifedha kutoka kwa wachangiaji mbalimbali na kuhasibu matumizi kuhakikisha kwamba zinaingizwa katika shughuli mbalimbali kwa manufaa ya wanachama wote.
k. Kuchukua hatua zote muhimu katika kuendeleza na kudumisha maelewano na mahusiano mazuri kati ya walipa kodi na mamlaka ya mapato
l. Kuandaa na kutekeleza tafiti mbalimbali, ukusanyaji wa taaarifa, mijadala na midahalo inayolenga kujenga uelewa wa mifumo ya kodi ili kuchochea mabadiliko ya mifumo hiyo nchini.
m. Kuongeza uelewa wa masuala ya kodi na kuhamasisha ulipaji kodi stahiki kwa hiari
n. Kubuni na kuwasilisha mapendekezo, sera na kampeni zinazolenga kupunguza mzigo wa kodi, kupunguza matumizi ya fedha za umma yasiyo na tija na kuongeza uwajibikaji wa serikali katika masuala ya fedha za walipakodi.