Events

TRA yatoa Elimu ya Mlipa kodi kwa waandishi DCPC, yashauri haya.

atika kuendelea kutoa Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA,) imekutana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) na kutoa Elimu ya Mlipa kodi ili kama waandishi watumie kalamu zao kufikisha elimu hiyo kwa wananchi na kujenga ari kwa wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari kwa maslahi ya Taifa ili liweze kutoa huduma stahiki kwa jamii.

Akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa semina hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi (TRA), Richard Kayombo amesema, wanaendelea kuelimisha jamii umuhimu wa ulipaji kodi na wataendelea kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo wahasibu na wafanyabiashara ikiwa ni mkakati wa Mamlaka hiyo wa kuwafikia wananchi wote na kuwajengea uelewa wa kulipa kodi kwa hiyari pasipo kufanya udanganyifu.

Advertisements
REPORT THIS AD

Aidha amesema, waandishi wa habari ni nyenzo muhimu kwa Mamlaka hiyo katika kuhakikisha kuwa elimu inawafikia watu wengi zaidi ili walipe kodi ambayo hutumika kwenye shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama barabara hospitali shule na masoko.