Events

TRA yawaandaa Wanafunzi kuhusu kodi, yafungua shindano kwa sekondari za Dar na Pwani.

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA), imesema wanafunzi ni kundi muhimu katika jamii ambalo linahitaji kufundishwa mambo mbalimbali kuhusiana na kodi ili kuwaongezea ufahamu ikiwemo kuwafanya kuwa wazalendo kwenye ulipaji wa kodi siku zijazo.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Kamishna mkuu wa TRA,Mche Hasani Mche,wakati akifungua shindano la vilabu vya kodi kwa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Aidha,Mche amesema mamlaka imeanzisha vilabu hivyo tangu mwaka 2008 ambapo kwa sasa inavilabu 292 vyenye jumla ya wanafunzi 48000 ambapo ni wanachama hai kwenye shule za Tanzania Bara ili kuwajengea uwezo na uzalendo kwa kuwaelimisha kuhusiana umuhimu wa kodi.

Hata hivyo,Mche ameongeza kuwa mamlaka hiyo itaendelea kutoa elimu kwa wananchi hususani wanafunzi wa shule za Sekondari ili kuendeleza utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari kwa wananchi na kuiwezesha serikali kutimiza majukumu yake kwa wananchi ikiwemo utoaji wa elimu bure,mikopo ya elimu ya juu,pamoja na ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo ambayo ni Miundominu ya Barabara,Reli,viwanja vya ndege,Hospital na Shule.

Kwa Upande wa Walimu ambao wamekuwa wanasimamia na kuwafundisha wanafunzi wenye vilabu hivyo vya kodi wamesema mashindano hayo yataisadia kuwa wawezesha wanafunzi kusambaza elimu ya kodi kwa walezi na wazazi wanaowazunguka na kuongeza uzalendo kwa Watanzania katika kulipo katika miaka ilayo.