EventsLatest NewsMediaspeechvideos

TATA yapendekeza mbinu ya kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari.

Chama cha walipakodi nchini, (TATA) kimeishauri serikali kumtambulisha Mlipa kodi kama Mfadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa nchini ili kuchochea ulipaji kodi.

Mwenyekiti wa TATA, Bw. Otieno Igogo amesema hivi karibuni kuwa mbinu hii imeonyesha mafanikio katika nchi zilizoendelea ambazo pia ni miongoni mwa nchi wanachama wa Chama cha Walipakodi Duniani (World Taxpayers Association – WTA).

“Iwapo serikali na Mamlaka ya mapato nchini, TRA itamtamblisha mlipakodi kama Mfadhili wa miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za kodi, hii itachochea ari ya ulipaji kodi miongoni mwa walipa kodi nchini” amesema Igogo.

Hivyo, ameshauri kwenye kila bango la mradi unaotekelezwa kwa fedha za kodi uandikwe “FEDHA ZA WALIPAKODI KAZINI’’ Hii italeta morali kwa walipakodi kuendelea kulipa kodi kwa uhiari wakitambua kuwa fedha zao zinatumika kuleta Maendeleo yao na kujenga uchumi wa Taifa.

Pendekezo hilo limekuja kufuatia hatua zilizochukuliwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA, Bw. Yusuph Mwenda katika kuhamasisha Walipakodi kuchangia maendeleo ya nchi kupitia ulipaji kodi kwa uhiari.

MLIPAKODI, MJENGA NCHI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *