Uncategorized

Walipa kodi wenye hadhi ya juu ambao wana mchango mkubwa katika mapato ya nchini sasa watahudumiwa katika ofisi maalum iliyopo katika jingo la Benjemin Mkapa towers lililopo mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.

Walipa kodi wenye hadhi ya juu ambao wana mchango mkubwa katika mapato ya nchini sasa watahudumiwa katika ofisi maalum iliyopo katika jingo la Benjemin Mkapa towers lililopo mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini, (TRA) Yusuph Mwenda alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa awali, (soft launch) wa ofisi hiyo.

Mwenda amesema ofisi hiyo itahudumia walipa kodi wenye hadhi ya juu ambao wako katika makundi manne ambayo ni wamiliki wa makampuni ambayo mauzo yao ni zaidi ya Sh20 bilioni kwa mwaka na wamiliki wa hisa katka soko la hisa la Dar es Salam, (DSE) zenye thamani ya zaidi ya Sh2.5 bilioni.

Makundi mengine mawili ni walipa kodi wenye ubia na makampuni unaozidi Sh20 bilioni kwa mwaka na wa mwisho viongozi wa mhimili mitatu na taasisi.

“Lengo ni kuongeza ufanisi na ulipaji wa kodi kwa hiari, tunataka tuwape huduma bora” amesema Mwenda.

Amesema mamlaka inafahamu viongozi wana mchango mkubwa na majukumu mengi hivyo lazima wawarahisishie zoezi la ulipaji wa kodi.

Sababu nyingine amesema ni usawa, wapo watu wanaofikiri kwamba kodi zipo kwa ajiliya watu wa chini peke yao.

Mpaka sasa ofisi hiyo ya hadhi ya juu imeanza na walipa kodi 158 ambapo kati yao walipa kodi wa miliki binafsi ni 111 na wengine 47 wa mihili mitatu.

“Huduma bora zitatolewa, zinazoendana na hadhi yao ili wapate muda wa kufikiri na kufungua makampuni zaidi ili serikali ipate kodi nyingi.

Mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *