Wasiliana na mshauri wa kisheria

WASILIANA NASI

Ikiwa una changamoto ya kikodi na hujaweza kuyatatua na TRA, basi huduma ya msaada wa kisheria ya TATA inaweza kukusaidia. Huduma yetu ni bure kwa ushauri, na ada ndogo kwa shida binafsi atachangia.

Kumbuka: Gharama za huduma zinategemea hitaji lako na wanachama wa TATA watatozwa kwa bei ya punguzo na wasio wanachama watatozwa kawaida 

Kipengele kipi kinachonifaa?

Ugumu wa kifedha pia unafahamika kama athari za kiuchumi na unajumuisha uharibifu wowote au kupoteza fedha katika kiwango chochote kile.

  • Utapoteza au hutaweza kupata chakula, kulipia huduma upatazo au kulipia usafiri kwenda kazini?
  • Je, utapata gharama kubwa kama vile ada za uwakilishi ili kukusaidia kupata nafuu?
  • Je utapata athari Mbaya kama vile upotevu wa Mapato, uharibifu wa ripoti ya mikopo, au uharibifu wowote ambao hauwezi kurudishwa katika hali ulivyokuwa awali.
 
 
 

 

 
Ikiwa jibu ni ndiyo kwa mojawapo ya maswali tajwa, TATA inaweza kukusaidia.

Suala la mfumo wa TRA pia linajulikana kama mzigo wa kimfumo ambao unaweza kujumuisha:

 

  • Ucheleweshaji lazima uwe zaidi ya siku 30 baada ya muda wa kawaida wa kuchakata ili kutatua tatizo linalohusiana na kodi. Kesi hizi hutokea wakati TRA inapotuma majibu mengi ya muda (Barua zinazowapa muda zaidi) na haichukui hatua nyingine kutatua masuala yako.
  • Ikiwa TRA ilitakiwa kukujibu au kushughulikia suala lako kwa tarehe maalum na hawajafanya hivyo, unastahili kupata usaidizi wa TATA.
  • Ikiwa mfumo au utratibu wa TRA umeshindwa kufanya kazi kama ilivyokusudiwa, au umeshindwa kutatua tatizo au mgogoro wako na TRA TATA inaweza kukusaidia..
Ikiwa jibu ni ndiyo kwa mojawapo ya maswali tajwa, TATA inaweza kukusaidia.

Jisajili kuwasiliana na mshauri wa kisheria, kupokea taarifa mpya juu ya unafuu na mabadiliko ya kodi yanayotolewa katika matangazo mbali mbali ya Chama cha Walipakodi Tanzania.