Kamishna TRA azindua SIKIKA APP.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda amezindua TRA SIKIKA APP ambayo itawezesha walipa kodi kuwasiliana moja kwa moja na ofisi ya Kamishna Mkuu ili kuweza kuwasilisha malalamiko na changamoto zao kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa TRA pamoja na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari imefanyika leo tarehe 9.8.2024, Jijini Dar es Salaam