Grassroots Campaign
Kampeni katika ngazi ya jamii zinalenga kuwajengea walipakodi uelewa wa maswala ya kodi, kuelimisha juu ya haki na wajibu wao ili kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika uandaaji na utekelezaji wa sera na sheria zinazohusu kodi kwa maslahi yao kiuchumi katika ngazi ya Jamii na Taifa kwa ujumla.Pia, kuhamasisha uwazi na usawa katika mifumo na viwango vya kodi pamoja na uwajibikaji katika matumizi stahiki ya fedha za walipakodi nchini, kupitia tafiti, ushawishi/uzengezi na kuhimiza mabadiliko ya sera na sharia za kodi.
Kwa kuzingatia kuwa mabadiliko huanza katika ngazi ya jamii, Chama cha Walipakodi Tanzania kimeandaa kampeni maalum kuhakikisha walipakodi wote wanapata Elimu itakayo wawezesha kufahamu haki na wajibu wao, kusimamia masuala ya kodi na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo nchini kupitia maboresho ya sera, mifumo na viwango wa kodi.
Mabadiliko huanza na sisi.
- KAMPENI ZINAZOENDELEA
- KAMPENI ZIJAZO
- BLACK BOOK
KAMPENI ZINAZOENDELEA