Dira na Dhamira

SISI NI AKINA NANI?
Sisi ni Chama cha Walipakodi Tanzania (TATA), ni asasi huru isiyo ya kibiashara, isiyoegemea upande wowote, inayojitolea kulinda haki za walipakodi na kuonesha umuhimu wa mchango wao kiuchumi na kijamii katika ujenzi wa Tanzania yenye ushindani .

MAJUKUMU YETU
Kazi ya Chama cha Walipakodi Tanzania (TATA) zinaongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997, inayoweka umuhimu mkubwa katika ushirikishwaji wa vikundi vya kijamii katika maendeleo ya nchi.
Asasi hii imeanzishwa kwa madhumuni ya kuwaleta pamoja walipakodi wa Tanzania Bara, kulinda na kutetea maslahi yao, kuwashauri na kuwafundisha kuhusu masuala ya kodi. kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari. Tunatetea kuhakikisha, kuwa walipakodi wanakuwa na uelewa mpana wa masuala ya kodi,vilevile kuhaikikisha sheria na sera za kodi, ni za haki na zinaeleweka kiasi ili kuwa na usawa na unafuu wa ulipaji kodi, ukusanyaji kodi wa kiungwana, kujenga mazingira ya maridhiano baina ya walipakodi na Mamlaka za mapato pamoja na kuhamasisha uwajibikaji wa serikali katika matumizi stahiki ya fedha zitokanazo na kodi zinazolipwa na wananchi.

Dira
Kuwa chama kinachoongoza kulinda na kutetea haki, wajibu na maadili ya Walipakodi nchini.

Dhamira

Kutetea, kulinda haki na maslahi ya walipakodi kwa kuwaleta pamoja, kuhimiza ulipaji kodi wa hiari, uwajibikaji wa serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi wote, kusaidia utatuzi wa migogoro ya kikodi, kufanya ushawishi na uzengezi serikalini ili kuboresha, kupunguza au kufuta sera za kodi, ada na tozo mbalimbali ambazo ni kero kwa mazingira ya kufanya biashara, utoaji wa taarifa na kufanya tafiti zinazolenga kupanua wigo wa kodi kwa madhumuni ya kuboresha mfumo wa kodi nchini.

Malengo Ya Chama
a. Kuwajengea walipakodi uelewa wa sera,mifumo na viwango vya kodi na kuchochea uwajibikaji wa Serikali katika kusimamia mapato na utoaji wa huduma za jamii.
b. Kulinda haki, wajibu na maadili ya walipakodi ili kuimarisha usawa masualaya kodi.
c. Kufanya tafiti, ukusanyaji wa takwimu na kushiriki katika mapendekezo ya uundaji wa sera na maboresho ya sheria za kodi.
d. Kujenga, kuimarisha na kuboresha uwezo wa chama katika kusimamia masuala ya Walipakodi.
e. Kudumisha uhusiano na kupaza sauti ya mlipakodi wa Tanzania katika majukwaa ya kodi duniani.