Kampeni

Chama cha Walipakodi Tanzania kimejikita katika uandaaji wa kampeni endelevu ili kushawishi watunga sera na wafanya maamuzi kuzingatia maslahi mapana ya walipakodi katika uandaaji na utekelezaji wa sera na sheria za kodi. Madhumuni ya kampeni hizi ni kuondoa taratibu za kodi zilizo kero zisizozingatia haki na usawa, kupitia ushahidi wa tafiti madhubuti na ushawishi wa sera ili kuimarisha ukusanyaji wa Mapato na udhibiti wa matumizi ya mapato ya serikali, pamoja na kuimarisha usawa na uwazi katika mifumo ya kodi nchini.

Kwanini ujiunge nasi!!

Kampeni hizi ni endelevu, na uzoefu wetu unaonyesha ili kuleta madadiliko na ufanisi katika mifumo ya kodi nchini, ni lazima Walipakodi wote tuungane ili kuwa na sauti moja inayotutambulisha na kushawishi viongozi kuzingatia maslahi yetu. Kupitia chama hiki sisi, Walipakodi tutaweza kupaza sauti zetu na kusikika.