TRA kuuona ‘moshi mweupe’ makusanyo ya kodi
Dar es Salaam. Endapo mwenendo wa makusanyo ya kodi utaendelea kuongezeka kama ilivyo sasa au kukusanya zaidi, Mamlaka ya mapato nchini (TRA) itaweka rekodi ya kukusanya zaidi ya malengo hivyo kuongeza kiwango cha utekelezeaji wa bajeti ya Serikali.
Mwaka 2023 bajeti inayopendekeza ni Sh44.38 trilioni na mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Sh31.38 sawa na asilimia 70.70, kati ya kiasi hicho Sh26.72 zinatarajiwa kukusanywa na TRA hususan katika kodi ya mapato, kodi ya ongezeko la thamani na ushuru wa bidhaa.