Latest Newsvideos

Zifahamu Kodi Zinazotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Ni wazi kuwa huduma kwa umma hazileti mkondo wa mapato ambao unaweza kgharamia huduma mbalimbali za umma. Kwa msingi huo, uboreshwaji wa uwezo wa sekta ya umma ili kuweza kuwa na matokeo mazuri itahitaji kuboresha ufanisi na kuongeza uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma, vile vile mapato makubwa ya serikali yatokanayo kodi. Kwa bahati mbaya watu wachache wanawajibika katika ulipaji wa kodi kutokana na kutokuaminika kwa taasisi za umma na ukosefu mkubwa wa uzoefu wa jinsi ya kulipa kodi kwa hiari. Vilevile, watu wengi na wafanyabiashara wana uelewa kidogo kuhusu haki na wajibu wao na wa kusimamia kodi na hawaoni uwiano wowote kati ya mapato \ na matumizi ya serikali.