EventsLatest NewsMafunzo na warsha mbalimbali

Mwaliko wa Mafunzo ya Mfumo Mpya wa Kodi za Ndani (IDRAS)

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawakaribisha wafanyabiashara, walipakodi na wadau wote wa kodi za ndani kuhudhuria mafunzo ya bure kuhusu IDRAS (Integrated Domestic Revenue Administration System) – mfumo mpya wa kisasa wa kusimamia kodi za ndani.

Ratiba ya Mafunzo:

Jumatano, 21 Januari 2026

Eneo: Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC)

Muda: Saa 3:00 asubuhi – 9:00 alasiri

Alhamisi, 22 Januari 2026

Eneo: Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City

Muda: Saa 3:00 asubuhi – 9:00 alasiri

Faida za kuhudhuria:

  • Jifunze jinsi ya kutumia mfumo mpya kwa urahisi na uwazi
  • Epuka changamoto na makosa ya kodi baadaye
  • Pata maelezo moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa TRA

Mafunzo haya ni bure kabisa na yanafaa kwa wafanyabiashara wote, waajiriwa na walipakodi binafsi.

Usikose fursa hii muhimu!

Njoo pamoja nasi tujenge taifa lenye uwajibikaji wa kodi.

Mlipakodi Mjenga nchi!

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *