Welcome
kwanini ujiunge na TATA
.
Chama cha Walipakodi Tanzania ni asasi huru ya kiraia, isiyoegemea upande wowote, iliyoanzishwa na kusajiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya sheria ya jamii (Sura ya 337), desemba 07,1999. Asasi hii ni ya kitaifa yenye ofisi yake Jijini Dar es Salaam.
.
Chama cha Walipakodi Tanzania ni miongoni mwa wanachama wa Chama cha Walipakodi Duniani – WTA chenye makao yake makuu Stockholm - Sweden. Kilichoanzishwa kwa lengo la kuleta pamoja vyama vya walipakodi duniani, ili kupeana ujuzi na uzoefu katika kulinda na kutetea maslahi ya walipakodi na kuinua uchumi wa nchi zao..
.
.
Chama cha Walipakodi Tanzania ni jukwaa maalum lenye lengo la kuwaleta pamoja walipakodi wote Tanzania bara , kwa madhumuni ya kuwajengea uelewa mpana wa aina , mifumo, sheria, na sera za kodi, kutatua changamoto za walipakodi kwa kushirikiana na serikali na wataalamu wa kodi, kuhamasisha ulipaji kodi kwa uhiari, kushauri na kutoa mapendekeo ya mabadiliko ya mifumo na sera za kodi zisizo rafiki ili kuleta ufanisi na uwazi katika ukusanyaji na matumizi ya fedha za kodi. Pia, kuhamasisha uwekezaji na ubunifu ili kupanua wigo wa kodi kwa lengo la kupunguza utitiri wa kodi ili kukuza uchumi wa mlipakodi mmoja mmoja na kuinua mapato ya kodi.
kwa kufanya yafuatayo;
- Kuwa na chombo kinacho waunganisha, watambulisha na kupaza sauti za walipakodi wa ngazi zote nchini.
- Kuunda mfumo utakaotoa fursa ya kukusanya maoni na changamoto za Walipakodi na kuziwasilisha kwenye mamlaka husika kwaajili ya utatuzi.
- Kuhakikisha kunakuwa na ushirikishwaji wa karibu wa makundi ya walipakodi katika uandaaji na utekelezaji wa sera na sheria za kodi.
- Kuandaa warsha, semina na midahalo yenye lengo la kutoa elimu, kupeana uzoefu, mbinu, na maarifa ya kushughulikia changamoto za kikodi. Kuandaa programu za usaidizi kwa ajili ya kuwajengea uwezo, kurahisisha mchakato wa ulipaji kodi na kushughulikia migogoro ya kodi.
Kwa ujumla Chama Kupitia ushawishi, vyombo vya habar na weledi wa wataalamu wetu, tutahakikisha kuwa changamoto za walipakodi zinapata suluhisho kwa uharaka na ufanisi, pamoja na kuhakikisha kuna kuwepo na maridhiano baina ya Walipakodi na Mamlaka za kodii nchini. Chama cha walipakodi ndiye mtetezi wa walipakodi, jiunge nasi kuleta mabadiliko nchini.
Mlipakodi, Mjenzi wa Taifa..